Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Kulogea kulogewa yai viza

$
0
0
Yai viza ni kitu kisichofaa kimekufa kinanuka hakina uhai...yai viza hutumiwa sana na wachawi wenye roho mbaya kuharibu maisha ya mtu..ni mojawapo wapo ya uchawi mbaya kabisa kulogewa nao
Mara nyingi hunuizua maneno kama haya ....kama hili yai lisivyo na uhai ....kama hili yai lisivyo na faida...kama hili yai linavyonuka...

Kisha baada ya manuizi hayo hupasuliwa njia panda ili litawanyike pande nane za uso wa dunia ili kila utakapoenda utakalofanya lisifanikiwe na uchukiwe na kukimbiwa na kila mtu....hata ulikuwa una mafanikio kiasi gani ghafla hujikuta unaanguka na nuksi balaa na mikosi kukuandama

NB: Sifundishi uchawi bali najaribu kuelezea ubaya wa kitu fulani kama hiki ili siku ikitokea kuna mtu kakuudhi usimfanyie jambo baya kama hili bali mwachie Mungu kwakuwa yeye ndio mwamuzi wa haki
Na wewe kama kuna mtu kajaribu kukufanyia hivi Usijaribu kwenda kwa waganga wa kienyeji kwakuwa huko unaenda kutafuta balaa zaidi la viapo na maagano ambavyo unaweza kuja kushindwa kuvitengua
Mwachie Mungu kwakuwa hata juju liweje huwa lina kikomo cha kuishi na kufanya kazi expire date

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>