Nina hakika gesi imekuwepo miaka mingi sana hapa Tanzania,na tunawataalamu na wanasiasa wengi tu hata baadhi ya wanajamii wanaojua kuwa gesi hiyo ilikuwepo,lakini huu ufundi wa kuijadili kwa sasa hadi itugawe watanzania, hao magwiji wa kujadili walikuwa wapi?na kwa sasa mjadala huu kupinduliwa na kuelekezwa kila upande mara leo uelekezwe kisiasa, mara leo kijamii zaidi, liko jambo hapa, Watanzania na hususa wasio wavivu wa kufikiri ni muda wa kuzama na kujiuliza kwanini suala la gesi igeuke shubiri kwa nchi? hebu utaifa uwe mbele na gesi tutumie kwa pamoja na kwa amani,ila mtu akiichepusha ikavuka mipaka ya nchi kienyeji hapo ndipo tufoke....Nawasilisha
↧