Katika ziara yako uliyoifanya siku za karibuni hapa wilaya ya Mpanda ulielezwa kwamba ukarabati wa stendi ya mjini Mpanda itawekwa lami pamoja na barabara zinazoingia maeneo ya stendi ambazo inafikia kilometa moja.Najua ulielezwa kwamba ndani ya siku thelathini barabara na stendi itakuwa imekamilika.Nakumbuka ulikuwa na mashaka sana kuhusu jambo hilo.Hebu muulize mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Mpanda kama hiyo barabara na stendi kama imekamilika hadi sasa barabara za kuingia stendi zimefungwa na stendi haitumiki hali hii imesababisha usumbufu mkubwa kwa abiria kutafuta mabasi ya usafiri wa kwenda maeneo mbalimbali ya mkoa wa Katavi kwani haijulikani mabasi yanapatikana wapi.Abiria wanazunguka na bodaboda kutafuta magari na kama ujuavyo unapozunguka sana na bodaboda na bei yake inapanda maradufu.Ni usumbufu mkubwa na kutowajibika kwa viongozi wa Halmashauri ambao wanadai eti walishalipa pesa yote kwa mkandarasi ili kuweka hiyo lami.Tunaomba ufuatilie jambo hili vinginevyo barabara zilizofungwa kuelekea stendi hasa vizuizi tutang'oa ili tupitishe mabasi yetu kubeba abiria.Tumechoshwa na uongo ulio bayana siku thelathini zimeisha bana!!
↧