Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Baba V: wa Mahusiano......Madame B nabwaga Manyanga kwa huyu.

$
0
0
Habarini za jioni Mabibi na Mabwana wa humu ChitChat.
Kiafya mimi ni Mzima na ninaendelea vizuri sana sana.
Kwako Baba V,
Mwenyekiti wa Tume ya Mahusiano Humu CC.
YAH: KUOMBA KUTENGUA NDOA YANGU NA Ndg: Arushaone.

Kichwa cha Habari Hapo Juu Chahusika,
Ndugu Mwenyekiti......kama utakumbuka kuwa nimekuwa nikikupigia simu kuhusu mtafaruku wa ndoa yangu na huyu aliyewahi kuwa Mume wangu Ndg: Arushaone, ni kuhusiana na Vipigo pamoja na Usaliti aliokuwa ananifanyia kila kukicha.

Mwenyekiti; nimekuwa nikipata vipigo pamoja na sintofahamu juu ya unakokwenda mshahara wake.
Wakati ananioa alinitamkia kuwa tutakuwa tunautumia mshahara wake tu,.....lakini siku hizi mambo na hali imebadilika sana, Pesa nikiomba sipewi na hata akinipa basi siku hiyo mtaa mzima watajua.
Hivyo sasa kwa Nakala hii ya Barua naomba mwenyekiti Uruhusu Ndoa hii ivunjike kwa Amani bila kutokea Uvunjifu wa Miili au mali.
Na Nitaomba baadhi ya nakala ya Barua hii iwafikie waume wake wenza aliowaacha kwenye Ndoa ambao ni Chimbuvu (huyu nae ana hati hati), Ben Saanane (huyu mpya), tedo na Chilli........mbali na waliopita Ruhazwe JR, Ruttashobolwa, BOBY na Chibolo.......nyie nafasi zimejaa.
ASANTE SANA Mwenyekiti @Baba V

CC: Mamndenyi, Judgement na wahusika wote wa Screening.
Somo wangu gfsonwin, Kungwi wangu snowhite na Nyakanaga wangu Lisa.

Pia habari hii iwafikie Rafiki zake wooooote wa Humu CC, Kama mlivyokuja kulila Pilau siku naolewa nae..........basi na mje kulila tena siku naachika nae.
Mke Mwenza Blaki Womani.........yamenishinda mie, nabwaga manyanga.
CC: Bishanga, Bujibuji, Vin Diesel, Kipaji Halisi, Nicas Mtei (kaka-binamu, yamenishinda), watu8 (shem yamenishinda) manoah, figganigga, Ruttashobolwa, KakaKiiza, Chachu Ombara, sosoliso, Kimbweka (nakudai), Mentor (mdogo wangu), Mtambuzi (pole sana kaka), @amu, Paloma, Jesca, cacico (umeniponza), KOKUTONA (me n'shajitoa), Arabela (nawaachieni), mwaJ, Zinduna (pacha,takutana Zenji), charminglady (usifanye huo uamuzi, CC: kaka Nicas Mtei) Evelyn Salt (now niko free, tupambe jukwaa letu sasa), dada white, FirstLady, King'asti (mndee,..otate naneeee... turudi zetu TA tukalime vitivo vya viazi), Kipipi.
Na Wengineoooooooo.

NAFASI IKO WAZI KWA MAKAKA WA CC ANAYEJIONA ANA SIFA YA KUZIBA PENGO LA Arushaone, kwani ameniachia Mali za Kutosha.

Wanachama wenzangu wa MKODOBWE.COM, itabidi tukutane ili tumsindikize Arushaone kwao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>