Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Kwa Mantiki Hii; CHADEMA ukombozi ni NDOTO.

$
0
0
Nasikitika kuona Majimbo mbalimbali hapa Dar es Salaam kuendelea kubweteka na kudhani Ukombozi umetimia.

Nashangaa kuona baadhi ya vikuruti/ vibaraka wakijiita MAKAMANDA wakati Kazi waitendayo ni kudhoofisha M4C.

Wapo wanaojitolea kwa Hali na Mali mpaka angalau CHADEMA ifikie lengo la kuwa na MATAWI kila KATA lakini viongozi wa Jimbo WANADHARAU hata wito wa WANAOJITOLEA.

Leo hii siamini Viongozi hao waliopewa majukumu ya Jimbo kama wanajua wajibu wao.

Nasikitika kuona Jimbo La KIGAMBONI likiongoza Migogoro ndani ya KATA zake kwa Makusudi au sijui wametumwa na CCM?

Nasikitika kuona Uongozi TAIFA kufumbia macho hujuma hizi ( ila Sidhani kama Wanazijua).

Kama Majimbo haya hayatasafishwa rasmi na kuzifuatilia KATA zote zilizo chini ya hayo MAJIMBO rasmi na kufufua matumaini mapya kwa WANANCHI na Wanachama waliokwisha kata Tamaa nacho baada ya KUDHARAULIWA, basi CHADEMA ukombozi hapa Dar Es Salaam Ni Ndoto.

Nasikitika sana!!!

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>