Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Upotoshaji-Hawa hawaruhusiwi na Rasimu

$
0
0
Leo,umeanza upotoshaji kuwa eti Marais wa zamani wa Tanzania,Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa,kwa mujibu wa Rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wataruhusiwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano kama wakipenda na kutaka.

Upotoshaji umeenda mbali zaidi na kudai kuwa hata Rais Jakaya Mrisho Kikwete naye aweza kugombea tena. Upotoshaji huu unaegemezwa kwenye Ibara ya 76,Ibara Ndogo ya 3 ya Rasimu husika. Upotoshaji huu umeandikwa na baadhi ya magazeti hapa nchini leo hii.

Ibara ya 76(3) inasomeka
(3)Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania Bara au Zanzibar hatapoteza sifa zakugombea na kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa sababu aliwahikushika nafasi ya madaraka ya Rais wa Tanzania Bara au Rais wa Zanzibar.(Msisitizo ni wangu)


Ni wazi kuwa,Ibara husika inataja mtu aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania Bara au Zanzibar. Kwa Katiba ya sasa,hakuna Rais wa Tanzania Bara. Lakini yupo Rais wa Zanzibar. Ndio kusema,kama Rasimu hii itadhinishwa na kuwa Katiba kamili,kutakuwa na Rais wa Tanzania Bara na Rais wa Zanzibar pamoja na Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ibara hii ya 76(3) itamhusu mtu yule tu ambaye atakuwa Rais wa Tanzania Bara au Zanzibar na baadaye mtu huyo kutaka kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mfano,Bwana X ni Rais wa Tanzania Bara na Bwana Y ni Rais wa Zanzibar. X na Y wataruhusiwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wakitaka na kupenda kufanya hivyo.


Kiuhalisia, Marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa na (Rais Kikwete) hawakuwahi kuwa Marais waTanzania Bara. Wao walikuwa na Kikwete bado ni Marais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania. Kwa Zanzibar,mambo ni tofauti. Wapo waliowahi kuwa Marais huko na ambao bado wako hai.Hao ni Mzee Aboud Jumbe Mwinyi,Komandoo Salmin Amour Jumaana Amani Abeid Karume. Hawa wote wanabebwa na Ibara ya 76(3) ya Rasimu.


Ni vyema vyombo vyote vya habari vilivyoripoti upotoshaji huu kesho vikaomba radhi na kuweka habari sahihi. Siku nyingine,hasa kwenye Tasnia ya Sheria,inashauriwa kuwa ni heri kuuliza kwanza kabla ya kuandikana kuchapisha habari za upotoshaji kama hizi.


Hatahivyo,Rasimu inaweza kubadilishwa na kuwa kama ilivyoripotiwa. Kwasasa, bado haiku hivyo. Si Mkapa,Mwinyi wala Kikwete watakaoruhusiwa kugombea tena Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Rasimu itabaki kama ilivyo sasa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>