Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, amelionya Jeshi la Polisi tabia ya kubambikia kesi wananchi kwa lengo la kupewa rushwa.
Waziri Nchimbi aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya kwanza ya askari polisi na Uhamiaji kwa mwaka 2012/13 ambapo alilitaja jeshi hilo kuwa moja kati ya taasisi zinazonuka rushwa.
Aidha alisema kuwa kutokana na hali hiyo, wananchi wamekuwa wakikosa imani na jeshi hilo na kwamba askari wanaofanya vitendo hivyo wanalitia doa jeshi hilo huku akiwataka askari wa kikosi cha usalama barabarani kutenda haki na kuacha kuomba rushwa.
Jeshi la polisi linaongoza kwa kubambikia watu kesi na pia ni moja kati ya taasisi zinazotajwa kunuka rushwa, kweli kiapo mlichokula cha kuwalinda wananchi na mali zao ndivyo mnavyofanya? Alihoji.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema amewabakiza chuoni askari 119 kuendelea na mafunzo kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na kufeli masomo yao kwa gharama za serikali.
Mwema alisema kati ya askari 3091 askari 119 watabaki chuoni hapo na endapo watafeli tena wataenda kufanya kazi zingine na endapo watakiuka taratibu za chuo watafukuzwa chuoni hapo.
Alisema kutokana na kuona dhamira yao ya kuwa walinzi wa amani, jeshi hilo limeona njia pekee ya kuwasaidia wanafunzi hao ni kuwapa mafunzo zaidi ili katika masomo waliyofeli waweze kuyafanyia mitihani na endapo watafeli Jeshi la Polisi litaangalia namna ya kuwasaidia.
Aidha katika hatua nyingine Mwema amewataka wale wote wanaotaka kumwaga damu kwenda kuchangia damu hizo katika hospitali mbalimbali kutokana na kuwa na upungufu wa damu hapa nchini.
Alisema jeshi lake halitamuonea haya wala aibu mtu yeyote atakayevuruga amani ya taifa hili kwa sababu zao binafsi ama za kisiasa au za kidini na kuwataka Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake kutii mamlaka ya dini au uongozi uliopo hapa nchini na hata katika maeneo wanamoishi.
Katika Mafunzo hayo yaliyofungwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kuhudhuriwa na mkuu wa chuo cha polisi nchini Kenya, Peter Kilonzo, yalienda sambamba na maonyesho ya umahiri katika kulinda amani.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI