Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Kwa ufisadi huu chadema imeisha jimbo la ilemela

$
0
0
Ndg mwana JF, siasa za Tanzania zinatupeleka wapi, ndg yako akipata nafasi ukoo mzima unashangilia, ninamshangaa bunge wa chadema ilemela kwa kupitia kaka yake Aitwaye CHARLES KIWIA wameshirikiana kudhurumu ardhi ya wananchi wa kijij cha LUTONGO mtaa wa CHAMIMBI , wananchi wamepeleka lalamiko lao kwa mtendaji wa kata ya sangabuye lakini wakaambiwa hawana chao na wasilalamike , matokeo yake charles kiwia anasema hakuna sehemu ya kumshitaki na akitaka anachukua ardhi ya eneo hilo bure, amezunguka kwa mwenyekiti wa kitongoji hicho ambaye anaitwa KUTENGWA akawashawishi wannchi hao waweke sahihi kuwa wamemuuzia eneo hilo, eneo la nusu eka anatoa elfu 30 za kitanzania na kwa sasa amezungushia uzio kuwa ndo mumiliki wa eneo hilo,kwa kisingizio kingine cha kuwa amepewa eneo hilo na halmasauri ya wilaya ya ilemela aweke BEACH,Hayo yote ni kuwanyayasa wananchi ambao hawajuwi sheria.Ninaziomba mamlaka husika kuangalia uwezekana wa kutatua hili suala ,kipindi cha mwalimu nyerere hayakuwepo haya , alidiriki kumweka ndani Mgiriki aliyetamba kwa kusema serikali ya Tanzania iko mfukoni kwake je watu kama charles kiwia tunawafanyaje kwa serikali ya sasa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>