CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
WILAYA YA ILEMELA.
TAARIFA KWA UMMA
CHADEMA Wilaya ya Ilemela tumekuwa katika mfululuzo wa mikutano pamoja na mbunge wa jimbo la Ilemela Mh Highness Kiwia. Mikutano hiyo ilihitimiswa tarehe 2/8/2013 kwa mkutano uliofanyika katika kiwanja cha minazi mitatu Kitangili.WILAYA YA ILEMELA.
TAARIFA KWA UMMA
Ujumbe mahsusi waliowasiliswa katika mikutano hiyo ulikuwa ni kwamba; uchaguzi wa meya wa Ilemela uliomweka Matata madarakani ulikiuka misingi ya sheria za nchi. Na swali liliulizwa,Je wanachi wakotayari kuendelea kuruhusu sheria za nchi kuvunjwa na wao kuendelea kukaa kimya?
Wananchi kwa ujumla walisema hawako tayari kuvumilia uvunjifu wa sheria na wakamtaka Mbunge aongoze maandamano ili kupeleka ujumbe kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Jana tarehe 7/8/2013, kamati ya utendaji ya wilaya ya Ilemela ilifanya kikao cha tathimini na kwa kauli moja wajumbe waliazimia mandamano yafanyike tarehe 15/8/2013. Kwa sasa maandalizi ya naendelea ikiwa ni pamoja na kutimiza taratibu za kisheria.
Kwa taarifa hii tunawaomba wananchi wote wajiandae kushiriki maandamano hayo ambayo ni muhimu sana kwa mustakabali wa maendeleo ya Ilemela.
ILEMELA AMANI, AMANI ILEMELA
CARLOS .N. MAJURA
KATIBU MWENEZI (W)
8/8/2013