Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Chopa ya Chadema yamchefua Godfrey Zambi

$
0
0
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi amekerwa na hatua ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutumia helikopta na kupandikiza maneno ya uongo kwa wananchi kuhusu mchakato wa Katiba Mpya. Kutokana na hali hiyo, amewataka wanachama wa CCM kutotishika na vitisho vinavyotolewa na wanasiasa kutoka CHADEMA, ambao hutumia muda mwingi kueneza propaganda dhidi ya CCM.

Kauli hiyo ameitoa jana, kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa, ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa inajadili ajenda ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Zambi, ambaye pia ni Mbunge wa Mbozi Mashariki (CCM), alisema kumekuwepo na vitisho vinavyotolewa na baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani na kudai kuwa CCM imeteka mchakato wa mabaraza ya Katiba Mpya ikiwa na lengo la kupitisha mapendekezo ya chama hicho.

“Vyama vya upinzani hasa CHADEMA kimekuwa kikizunguka na helikopta na kufanya mikutano mbalimbali ikiwa na lengo la kueneza chuki kwa wananchi wakatae mabaraza haya na kushindwa kutoa mapendekezo yao,” alisema.

Alisema, utoaji maoni kwenye mabaraza umekuwa ukifuata taratibu na mifumo iliyowekwa na Tume ya Katiba, hivyo CCM ni moja ya Taasisi ambayo nayo ina haki ya kutoa maoni yake kwa mujibu wa sheria.

“Tume ya Katiba inapaswa kufuata taratibu zake zile zile na kupuuza maneno yanayotolewa na wanasiasa kwenye majukwaa ambao muda mwingi wamekuwa wakisema uongo kwa wananchi,” alisema Zambi.

Alisema, CCM bado ina nafasi kubwa ya kutoa maoni yake kuhusu mapendekezo ya rasimu ya Katiba, kwani asilimia kubwa ya wapinzani wanazungumzia juu ya kuvunja Muungano uliopo sasa.

Hata hivyo aliwataka wanachama wa chama hicho kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao, ikiwemo kuvunja makundi yote na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka 2014.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>