Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Kulikoni treni ya Mwakyembe?

$
0
0
Leo asubuhi nilikuwemo kwenye treni inayotambulika sana hapa jijini Dar, kama treni ya Mwakyembe, ambapo treni hiyo iliondoka kituo cha mwisho cha Ubungo maziwa saa 3 asubuhi badala ya saa 2.30 kama ilivyo kwenye ratiba yake. Abiria tulipohoji sababu ya kuchelewa kuondoka kwenye kituo hicho, tukaambiwa kumetokana na sababu ya kutokea kwa ajali iliyotokea asubuhi ya leo, majira ya kama saa 1 kwenye kituo cha Mabibo, ambapo gari ndogo iliigonga treni hiyo. Tuliendelea na safari hiyo hadi kituo cha Buguruni kwa Bakhresa, lakini mara tu baada ya kutoka kituo cha Bakhresa, baada tu ya mwendo mfupi, treni hiyo ikasimama ghafla mahali ambapo siyo kituo chake,abiria tukaanza kujiuliza kulikoni? hatukuweza kuelewa nini kinaendelea. Ingawa treni hiyo inazo spika ambazo wafanyakazi wa treni huzitumia kuwatangazia abiria kila tunapofika kituoni, lakini pale tuliposimama, hakukutolewa tangazo lolote, badala yake wafanyakazi hao wakafungulia sauti kubwa muziki na matangazo ya radio ya Clouds! Tulisimama pale zaidi ya nusu saa, ndipo abiria walipochachamaa kuwaambia wafanyakazi wa treni hiyo waeleze nini kinaendelea, ndipo likatolewa tangazo kupitia kwenye spika hizo, wakitueleza kuwa treni lina matatizo ya kiufundi kwenye injini, kwa hiyo wameagiza waletewe injini nyingine kutoka stesheni kuu,baada ya muda mfupi injini ikaja, ikaungwa na tukaendelea na safari. Lakini kwa hali yoyote ile, kuchelewa huko kwa hiyo treni kulisababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wa treni hiyo, ambao mambo yao mengi yaliharibika kutokana na kuchelewa maeneo ya kazi, waliyokuwa wanakwenda. Sasa swali tunalojiuliza abiria wa treni hiyo, tunafahamu kuwa siku ya Jumapili, treni hiyo inasitisha safari za kusafirisha abiria, ili lifanyiwe service. Ni kwa nini hilo halifanyiki hadi kusababisha injini inazimika njiani na kusababisha usumbufu mkubwa wa abiria? Jambo lingine linalotukera abiria,ni kwa nini hawakutumia speakers za kwenye treni kutoa taarifa mapema kuhusu kuharibika kwa treni hiyo? Kero nyingine kubwa ambayo abiria wengi huwa tunalalamika, ni kwa nini treni hiyo inapenda kufungulia radio ya Clouds, ambayo haina matangazo yoyote ya maana kama vile taarifa za habari ambazo zingekuwa na manufaa sana kwa abiria Na badala yake treni hiyo imekuwa ikipendelea kufungulia Clouds radio, ambayo imejikita zaidi kwenye kutangaza, umbeya na mipasho?! Tunajua treni ya Mwakyembe ilianza vizuri sana, na ilishajizolea mashabiki wengi sana ambao walishaacha kupanda daladala na sasa wanapanda treni hiyo. Lakini sisi abiria tunawatahadharisha, tutalazimika kutafakari upya, kama treni hiyo wataendelea kuiendesha 'kihunihuni' kama walivyoanza sasa, abiria tutalazimika kurudi kwenye usafiri tuliouacha kipindi kirefu sasa, wa 'wahuni wenzao' wa daladala!!

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>