Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Kesi inayomkabili Mchungaji Daniel Mwasumbi imeendelea leo katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya ambapo utatuzi wa kisheria ulifanyika na hakimu wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo anyesikiliza kesi hiyo alitoa ufafanuzi wa kisheria
Ndeuruo amesema mahakamani hapo kuwa miongoni mwa sababu zilizopelekea mahakama kukataa kupokea sampuli ya vinasaba DNA ni pamoja na mtuhumiwa kutosaini katika barua ya mrakibu wa polisi , mshtakiwa kutosomewa haki zake kabla ya kuchukuliwa vipimo ,mshtakiwa kutokupewa nakala ya majibu kwa mujibu kifungu cha vinasaba kifungu cha 25 kifungu kidogo na cha pili (c) kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002
Pamoja na Mlalaikaji Neema Ben kutoa vielezo mahakamani ambavyo ni watoto wake Irene na Johnson mahakama imesema haiko tayari kupokea vina saba kutokana na kutokukamilika kwa taratibu za kisheria
Wakili wa serikali Achirey Mulisa na wakili wa utetezi Mkumbe wamekubaliana na hatua iliyofikiwa na hakimu wa mahakama hiyo ambapo kesi hiyo itatajwa tena march 7 mwaka huu.
Siku ya jana, sakata hilo la mchungaji DANIEL MWASUMBI limeingia katika sura mpaya baada ya mchungaji huyo kutokufika mahakani kwa kusingizia ugonjwa
akisoma hati ya ya mashtaka mwendesha mastaka wa mahakama hiyo ACHIREI MULISA mbele ya hakimu GILBERT NDEURUO amesema hakubaliani na hoja ya wakili wa mtuhumiwa wakili MKUMBE kuwa mtuhumiwa ni mgonjwa licha ya kuwasilishwa cheti cha zahanati ya ebeneza iliyoko kabwe jijini mbeya
Kufuatia taarifa hiyo wakili huyo aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa muda na kuamua kufuatilia hadi katika zahanati hiyo ambapo dactari YUSUFU YASINI SENTI alikiri kutoa cheti bila kuonana na mgonjwa ambapo hata jina halikuorodheshwa katika vitabu vya zahanati
Baada ya dactari kukiri wakili alimuomba wakili wake pamoja na mdhamini kumleta mtuhumiwa mahakamani mara moja ambapo aliletwa na kesi kuendelea katika mahakama ya siri na ushaidi kuanza kutolewa
Miongoni mwa waliotoa ushaidi ni pamoja daktari aliyepima vinasaba FIDELIS SEGUMBA na mwanafunzi wa shule ya sekondari ITENDE ambaye anadaiwa kuzaa na mchungaji huyo na kuleta vielelezo wakiwemo watoto wawili wa kike na wa kiume ambao inadaiwa kuzaa na mchungaji MWASUMBI
Hata hivyo kulizuka ubishani wa kisheria ambapo wakili wa mtuhumiwa alipinga kupokelewa kwa vipimo hivyo mbele ya mahakama na kudai kuwa taratibu za kisheria hazikufuatwa hali iliyosababisha kuairishwa kwa kesi hiyo ambapo kesi hiyo itasomwa tena leo na hakimu kuwagiza upande wa serikali kuleta barua ya uthibitisho