Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa Umma imesema wakati wowote katika wiki ya kwanza ya Julai, ratiba na majina ya waliokidhi vigezo kwa ajili ya usaili kwa matangazo ya kazi yaliyotolewa kwa lugha ya Kiswahili tarehe 26 Machi, 2013 itatolewa
Hayo yamesemwa na sekretarieti wakati ikijibu hoja za wadau mbalimbali kwa mwezi Mei na Juni 2013
'Ni kweli tulitoa matangazo mawili ya nafasi wazi za kazi ambapo kwa tangazo la Kiingereza mchakato wake umeshakamilika, ambapo tunategemea kwa tangazo la kazi lililokuwa limetolewa kwa lugha ya Kiswahili tarehe 26 Machi,2013 kwa Kada mbalimbali usaili wake unatarajiwa kufanyika muda wowote kuanzia mwezi Julai, 2013. Hivyo,Katibu wa Sekretarieti ya Ajira amewataka wale wote ambao walituma maombi yao watambue kuwa ratiba na majina ya waliokidhi vigezo yatatolewa katika mtandao wa Sekretarieti ya Ajira wiki ya kwanza ya mwezi Julai, 2013,hivyo waendelee kutembelea mtandao huo ili kufahamu sehemu, tarehe na siku ya usaili husika maana baadhi ya saili hizo zitaendeshwa mikoani hasa kwa wale wote waliotumia anuani za mikoani hususan waombaji wa kazi kwa fursa za kada za chini' Imesema taarifa hiyo