Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

News Alert: Kafulila amvaa cag!

$
0
0
1. CAG Akabidhi ripoti ya uchunguzi wa ufisadi wa 200bn kabla hajacha Ofisi siku ya ijumaa. Hii ni kwasababu yeye mwenyewe kabla hajagizwa na Bunge aliomba siku45 marchi20 na leo zaidi ya siku 160 hajakabidhi ripoti bila taarifa yoyote. Majibu anayotoa kuwa watafanya waliobaki yanatia mashaka hasa ukizingatia muda uliokwisha mpaka sasa. Anaposema kazi hii ni sawa na majukumu mengine ya kawaida ni kielelezo cha kukimbia wajibu wake katika suala hili tete ambalo limepelekea mpaka sasa nchi wahisani wasichangie bajeti kusubiri uchunguzi na hatua. CAG Utouh ni moja wa wakaguzi ambao sasa anakagua Hesabu za UN, hii ni sifa kubwa sana ambayo hatutegemei awe mwoga na akimbie majukumu kiasi hiki. Ni kielelezo kuwa kuna dalili za uchakachuaji kwenye uchunguzi huu.

2. Akaunti ya VIP mkombozi bank ilipaswa kufungwa mpaka uchunguzi ukamilike kwani ni mfaidika wa hela za escrow zinazochunguzwa. Hiwezekani Bank ya Ulaya imesimamisha Akaunt ya VIP uholanzi kwa mashaka ya kupokea hela zinazochunguzwa za escrow lakn Tanzania bado VIP haijafungwa kusubiri uchunguzi

3. Taarifa zilizopo PCCB wameshakabidhi report Ikulu badala ya Bunge wakati uchunguzi ulikuwa kwa azimio la Bunge. Hii ni kinyume cha utawala bora na ni mwanya wa uchakachuaji wa report kama ilibotokea mwaka 2000 ambapo Report ya PCCB kuhusu wahusika waliongiza nchi kwenye mkataba mbovu wa IPTL walifichwa na Ikulu na kusababisha nchi kuendelea na mkataba wa kinyonyaji wa miaka 20.

4. Serkali ilipaswa kusimamisha malipo ya capacity charge ya 4bn kila mwezi mpaka uchunguzi ukamilike kwani malipo hayo ndio yanayochunguzwa

5. Vigogo wa serikali, Bunge na Mahakama wanaotajwa kulipwa fedha kupitia akaunt ya VIP wanapaswa kuchunguzwa na PCCB kwakuwa akaunt hiyo ilipokea fedha za escrow. Hivyo ni wito wangu kwa PCCB imuhoji Prof Tibaijuka kwakuwa amekiri akipokea.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>