Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

alinilazimisha nitoe mimba

$
0
0
nilikuwa na mpenzi wangu miezi miwili kabla ya tarehe tuliyopanga wazazi wake waje kujitambulisha nikapata ujauzito wake. hapo ndipo nikamfahamu alivyo. alinilazimisha nitoe mimba nilivyo kataa akanambia "kama mimba ni yangu lazima utoe usipotoa ni ujeuri wako labda kama una jamaa mwingine umezaa naye" alinitukana sana mimba ilikuwa inasumbua nalazwa hospital karibu kila week hakujali wazaz wake walijaribu kumshaur ikashindikana kwakuwa hatujawah gombana. nikakubaliana na hali nakukubali kibuti. katika kugombana nikagundua nimshirikina kupindukia na nimganga wakienyeji anaagua kabisa na nimsomi wa chuo kikuu kaajiriwa ni mwalimu.alishaniomba msamaha sana turudiane ila kwa tabia zake moyo wangu umemchukia nakumfuta kabisa. ila naumia je mtoto wangu huyu nlozaa hata akiwa mkubwa akitaka kwenda kumsalimu baba yake huyu mwalimu a.k.a mganga wa kienyeji hawezi kumfanyia mambo mabaya na hivi hakutaka azaliwe. maskin binti yangu ninavyompenda

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>