Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Daima nitaichukia CCM na serikali yake!

$
0
0
Binafsi nasema nitakichuki hiki chama maisha yangu yote mpaka siku naingia kaburini.

Inasikitisha na kuumiza kuona kundi la watu wachache wanajineemesha na kuishi kama wako peponi huku wengine wakifa kwa njaa na magonjwa.

Inasikitisha wengine wanalipwa 300,000 kwa siku na mwingine analipwa 170,000 kwa mwezi.

Inasikitisha na kuumiza kuona watu wamejinufaisha na madini yetu huku sisi masikini tukiambulia kuona mashimo na uharibifu mkubwa wa mazingira.

Inasikitisha na kuumizi kuona walivyojenga mahekalu huku wengine hata nyumba za nyasi zinatushinda.

Inaumiza sana kuona watanzania wanaomba msaada wa matibabu kupelekwa nje ya nchi wakati wao wakiuugua wanapenda ndege kwenda India na kwingineko kwa matibabu.

Inasikitisha kuona wamejimilikisha nyumba za serikali wakati mfanyakazi anaelipwa mshahara mdogo akishindwa kulipa kodi kwenye nyumba za watu binafsi.

Inasikitisha na kuumiza kuona viongozi wanaotumiwa kwa wizi na ufisadi wa mabilioni wakiachwa madarakani na wanaojiuzulu hawafikishwa katika vyombo vya sheria.

Inasikitisha kuona watumishi wa umma wanadai malimbikizo ya stahiki zao huku mamilioni yakitumika kugharamia safari za viongozi zisizokwisha nje ya nchi.

Anyway, ipo siku tutapata uhuru wa kweli baada ya mkoloni kuondoka mwaka 1961.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12945

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>